NB-PICHA HAIHUSIANI NA HABARI HAPA CHINI |
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino ametekwa katika wilaya ya Chato mkoa wa Geita.
Polisi
wameeleza kuwa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Yohana Bahati mwenye
umri wa mwaka mmoja alitekwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana jana
usiku.
Kwa
mujibu wa taarifa za mwandishi kutoka eneo hilo Renatus Masuguliko,
polisi wamefika eneo la tukio na kuanza msako mkali dhidi ya watu
wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho.
Habari
zinasema watu waliokuwa na silaha za jadi waliwaweka chini ya ulinzi
Bahati Misalaba na mkewe ambao ni wazazi wa mtoto albino ambaye
walimteka na kutoweka naye.
Familia
hii pia ina watoto wengine wawili wenye ulemavu wa ngozi, Tabu Bahati
mwenye umri wa miaka miwili na Shida Bahati mwenye miaka kumi na mmoja
ambao walinusurika kuchukuliwa na watu hao kwa sababu wakati unyama huo
ukitendeka nyumbani kwao hawakuwepo walikwenda kucheza kwa majirani zao.
Mama wa mtoto huyo alijeruhiwa vibaya wakati akimpigania mtoto wake asichukuliwe na watu hao.
Matukio
ya kuwaua na kuchukua viungo vya albino yaliyasambaa katika mikoa ya
kanda ya Ziwa kutokana na imani za kishirikina kuwa viungo vya watu hao
vingeweza kuwapatia utajiri na mafanikio mengine katika maisha yao,
jambo ambalo ni upuuzi mtupu.
Social Plugin