Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUHUSU WATU WANAOSAMBAZA PICHA NA VIDEO ZA UTUPU ZA WAPENZI WAO

guilty2
Kumekuwa na ishu ya kuvuja kwa picha za utupu za watu mbalimbali ikiwemo mastaa kwenye mitandao, wakati mwingine tumesikia wenye picha hizo wakilalamika kwamba zimevujishwa na wapenzi wao wa zamani.


Kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya aina hii, Uingereza wamepitisha Sheria, iwapo ukivujisha picha za utupu za mtu yoyote bila idhini yake ni kifungo cha miaka miwili pamoja na faini.

Kwa Marekani hii Sheria imepitishwa kwenye majimbo 12 tayari.

Ishu za kuvujisha picha, video zipo hata Bongo pia, unadhani ikipitishwa Sheria itasaidia kukomesha hii?

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com