Kipaji cha mtoto huanza kuonekana
taratibu wakati anaendelea kukua, mara nyingi wazazi huwa wanakua wa
kwanza zazi ndio wakati wa kutambua mwanaye anataka nini kwa maisha yake
ya baadaye lakini kipaji cha mtoto Esther Okade kimekua cha ajabu na kumshangaza kila mmoja.
Unaweza usiamini lakini huu ni ukweli, Esther
ambaye ana umri wa miaka 10 amejiunga na masomo ya chuo kikuu huria cha
Uingereza miezi mitatu iliyopita akisomea shahada ya hesabu.
Mtoto huyo ambaye anatokea katika mji wa Walsaw uliopo Midlands, Uingereza sio
mtoto pekee mwenye kipaji cha aina yake, mdogo wake wa kiume mwenye
miaka sita anasoma masomo ya kidato cha tano katika mchepuo wa hesabu.
Pamoja na Esther kudahiliwa miezi mitatu iliyopita ameonekana kufanya vizuri kuzidi wenzake darasani.
Mama yake Esther aitwaye Ife anasema
kitendo cha mwanae kujiunga chuo kikuu kilikuwa la kushangaza kutokana
na umri wake kuwa mdogo lakini mwenyewe alijiamini na kuona anaweza.
“Tangu akiwa na miaka saba alikuwa
na shauku ya kujiunga na chuo kikuu ili atimize ndoto zake, alikua na
kipaji cha aina yake darasani na baada ya miaka mitatu aliuliza tena
ikabidi tumpeleke ili kuona kama kweli atamudu“– amenukuliwa Ife, mama wa Esther.
Historia inaonyesha kuwa Esther si wa kwanza kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri mdogo, mwaka 1981 mtoto aitwaye Ruth Lawrance alijiunga na chuo kikuu cha Oxford na kuhitimu mwaka 1985.
Social Plugin