KUTOKA BUNGENI LEO,WABUNGE WAJADILI KUHUSU MOVIE ZA TANZANIA

Ray II
Kikao cha Bunge kimeendelea leo Dodoma, wakati wa maswali na majibu moja ya ishu ambayo iliulizwa ni kuhusu Serikali inafanya jitihada gani kuzuia movie ambazo ziko kinyume na maadili ya Tanzania.
 
“Serikali imeshafanya tafiti zozote zile zinazoonyesha athari ni kwa kiasi gani utamaduni wetu umeathirika? kwa kuwa kasi ya utandawazi ni kubwa sana sana na kasi ya Serikali kuwisha au kuimarisha hizo sera na sheria ni ndogo sana,na kundi linaloathirika ni vijana,Serikali haioni kasi hiyo ndogo waliyonayo itaangamiza nguvu kazi ya Taifa na kupoteza tamaduni zetu zote?”– Mbunge Amina Mwidau.

Akijibu kuhusu suala hilo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na  Michezo Juma Nkamia amesema; “Serikali kwa upande wake tuna vyombo mbalimbali vinavyosimamia jambo hili,kwanza ni bodi ya filamu ambayo husimamia filamu zinazotoka nje na ndani ya nchi,ili kuhakikisha zinazoingia kwenye soko zinafata maadili,tuna Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kazi yake ni kuhakikisha lugha iko sawa, lakini pia tuna kamati ta maudhui ipo chini ya TCRA  kazi yake ni kusimamia maudhui
 
Baada ya majibu hayo Mbunge Maryam Msabaha aliuliza; “Wasanii wengi wanaiga mambo ya kimagharibi na filamu zao nyingi wanazozionyesha  zinakiuka maadili ya Mtanzania, Je Serikali inachukua hatua gani kuzuia filamu hizo?”

Hakuna filamu inayoingia sokoni bila kutizamwa na kuruhusiw na bodi ya filamu na inahakikisha haiharibu utamaduni wa mtanzania,tunajua zipo zinazoingia kwa njia ya panya lakini kuna njia ambazo tunatumia kuwakamata, zipo  filamu  nyingine zimeteketezwa kutokana na kutoridhika nazo“– Juma Nkamia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post