Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Rasi FM ya Dodoma Oscar Kiwanga Kahuka akizungumza na bibi anayedaiwa kubariki ndoa ya mtoto mdogo huko Dodoma |
Mwanaume mmoja kwa jina la Joshua
Mnhamba mwenye umri wa miaka 27 Mkazi wa Ibihwa wilayani Bahi mkoani Dodoma
anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa kuishi na mtoto mwenye umri wa miaka kumi
kama mke wake baada ya moto huyo kuozeshwa na bibi yake.
Mwanaume huyo alifunga ndoa na Neema Stephano mwenye umri wa miaka 10 mnamo Januaryi 27 mwaka huu huko kijiji cha Ibihwa kwa lazima, ambapo bibi wa msichana huyo Bibi Ntolwa Malambu Mpondo akishuhudia tukio hilo na mashahidi wengine watatu.
Hata hivyo alipoulizwa bibi yake amekana kuwa yeye hahusiki na tukio hilo huku akiwatupia mzigo huo wazazi wa mtoto huyo kwa kudai wao ndiyo waliomuoza na yeye hana mamlaka ya kuingilia familia ya watu.
Kaimu mtendaji wa kijiji cha ibihwa
Noro Said Noro amelaani kitendo hicho huku akiwataka wanakikiji kutoa taarifa
katika matukio yote ya namna hiyo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua
stahiki.
Tayari jeshi la polisi linamshikilia mwanamme huyo kwa mahojiano zaidi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Na Josephine Charles Malunde1 blog-
Dodoma
Social Plugin