Duniani kuna afua mbili, Kufa au kupona.
Jamii nyingi hutofautiana jinsi wanavyomkaribisha mwana wao humu duniani na pia jinsi wanavyomuaga anapotangulia mbele ya haki.
Katika jamii nyingi duniani, kuna tamaduni tofauti za kuomboleza,kuadhimisha, na kuwazika wapendwa wao.
Jamii
moja inayoonesha mbinu za kipekee za kuomboleza na ya kupigiwa mfano ni
ile ya Dani, iliyoko Magharibi mwa Papua New Guinea.
Tabaka hilo
huwa linaomboleza wapendwa wao kwa kujikata vidole vyao, kama
dhihirisho ya kuwa kweli ulikuwa unampenda yule aliyeaga dunia !
Tamaduni
hiyo ambayo inaonekana ya kutisha imekita mizizi sana miongoni mwao na
si ajabu unapotembeatembea kijijini utashangaa kuwaona watu waliokatwa
viganja vyao vikaisha.
Hilo likiwa dhirisho kuwa amefiwa na wapendwa wake.
Wakaazi
hao wa bonde la Baliem wamekuwa wakifuata tamaduni hiyo kwa miaka na
mikaka na hivyo sio jambo ambalo linawezatoweka kwa haraka.
Mtindo huu hufanyika kwa yeyote ule mwenye uhusiano na marehemu, wakiwajumuisha wazee, wanawake na hata watoto.
Utamaduni
huo huanza kwa ibada kwa minajili ya kufukuza mapepo ya marehemu, na
pia kama njia ya kutumia maumivu ya kimwili kuonyesha huzini na mateso
ya kufiwa.
Vidole vyao hufungwa kwa kamba, kisha kukatwa na shoka, vipande vilivyokatwa huchomwa kwa moto na jivu huhifadhiwa.
Wakati mwengine vipande hivyo huzikwa pamoja na marehemu.
Vidole hukatwa hususan kuonyesha upendo kwa marehemu.
Kwa mfano, mume au mke hukatwa kidole na kukizika pamoja na maiti ya mume au mke wake, kama ishara ya upendo.
Haijabainika ni kidole kipi kinachopendelewa ama ishara ya mwili na roho kuunganishwa pamoja milele.
Idadi ya vidole vinavyokatwa ni shara ya wale waliofiwa na waliopendwa katika jamii.
Jitihada
zimeanza kufanywa ilikusimamisha matambiko ambayo yanahusisha utamaduni
huu ambao madhara yake yanabainika katika jimbo lote wakaoishi jamii
hii.
Je tamaduni zako zinakushurutisha kufanya nini ilikumuaga mpendwa wako ?
Via>>BBC