Maelfu
ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wamejitokeza kumzika
aliyekuwa mchezaji nguli wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na
klabu ya Simba Christopher Alex Masawe aliyefariki dunia Jumapili
iliyopita katika hospitali ya Milembe kufuatia kuugua ugonjwa wa kifua
kikuu kwa muda mrefu.
Christopha Alex Masawe ambaye moja kati ya matukio atakayokumbukwa
na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi ni mkwaju wa mwisho wa penalt
ulioyiondosha katika mashindano ya klabu bingwa barani afrika timu
Zamalek ya Misri ambayo ilikuwa inashikilia ubingwa wa afrika mwaka
2003.
Mwili wa nguli huyo umezikwa katika makaburi ya Nkuhungu na maelfu
ya waombolezaji huku baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza nae enzi za
soka lake akiwemo mlinda mlango Juma Kaseja na mlinzi Boniphace Pawasa
pamoja na wadau wa soka nchini wakazungumzia kile walichokifahamu kuhusu
nyota huyu aliyezimika.
Social Plugin