Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Hapa!! SHULE 10 BORA KWA UFAULU,10 ZA MWISHO NA WANAFUNZI 10 BORA ZAIDI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014



Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.



Shule kongwe na za vipaji hoi
Shule za vipaji kama Ilboru, Mzumbe, Msalato, Kilakala, Tabora Boys, Kibaha na Tabora Girls na Shule kongwe zinazomilikiwa na Serikali kama Pugu, Zanaki, Bwiru Boys, Minaki, Azania na Jangwani, kwa mara nyingine zimeshindwa kufua dafu kwa shule za binafsi.
Katika orodha ya shule 10 bora shule binafsi zilizotamba katika matokeo hayo ni 
Kaizirege (Kagera)
 Mwanza Alliance (Mwanza)
 Marian Boys (Pwani)
 St. Francis Girls (Mbeya)
 Abbey (Mtwara)
Feza Girls (Dar es Salaam)
Canossa (Dar es Salaam)
 Bethel Sabs Girls (Iringa)
Marian Girls (Pwani) na 
 Feza Boys (Dar es Salaam).
Shule 10 za mwisho ni 
Manolo (Tanga)
Chokocho (Pemba)
Kwaluguru (Tanga)
Relini (Dar es Salaam)
 Mashindei (Tanga)
 Njelekela Islamic Seminari (Kigoma)
 Vudee (Kilimanjaro)
Mnazi (Tanga)
 Ruhembe (Morogoro) na 
 Magoma (Tanga).
Watahiniwa 10 bora kitaifa
Dk Msonde aliwataja wanafunzi 10 bora kitaifa kuwa ni Nyakaho Marungu (Baobab), Elton Jacob (Feza Boys), Samwel Adam (Marian Boys), Fainess Mwakisimba (St. Francis Girls), Mugisha Lukambuzi (Bendel Memorial), Paul Jijimya (Marian Boys), Angel Mcharo (St. Francis Girls), Atuganile Jimmy (Canossa), Jenifa Mcharo (St. Francis Girls) na Mahmoud Bakili (Feza Boys).
Wasichana 10 bora kitaifa
Katika matokeo hayo mwanafunzi bora kwa wasichana ni Nyakaho Marungu (Baobab), aliyefuatiwa na Fainess Mwakisisimba (St. Francis Girls), Angel Mcharo (St. Francis Girls), Atuganile Jimmy (Canossa), Jenifa Mcharo (St. Francis Girls), Levina Ndamugoba (Msalato), Veronica Wambura (Canossa), Sifaely Mtaita (St Maris Mazinde Juu), Catherine Ritte (St. Francis Girls) na Anastazia Kabelinde (Kaizerege).
Wavulana 10 bora
Dk Msonde alimtangaza kinara kwa wavulana kuwa ni Elton Jacob (Feza Boys) akifuatiwa na Samwel Adam (Marian Boys), Mugisha Lukambuzi (Bendel Memorial), Paul Jijimya (Marian Boys), Mahmoud Bakili (Feza Boys), Amani Andrea (Moshi Technical), Mahmoud Msangi, Elias Kalembo, Haji Gonga na Kelvin Sessan wote kutoka Feza Boys.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com