Watu wanawapenda mastaa, wapo
wanaowapenda mpaka wanatamani wafanane nao, mara nyingi tumekutana na
hizi story za watu ambao wamekuwa wakifanya majaribio ya kujibadilisha
muonekano, maumbile yani ili tu afanane na staa wake anayempenda.
Jordan James alitumia dola 150,000 (zaidi ya mil 270/-) ili kujibadilisha afanane na Kim Kardashian, safari hii ni Adam Guerra ambaye yeye jitihada zake alikuwa akizifanya ili afanane na Madonna.
Pesa aliyotumia ni paundi 75,000/- (sawa
na mil. 210/-) na kutokana na ‘ukarabati’ ambao anataka kuendelea
kuufanya kwenye mwili wake mpaka zoezi likamilike kiasi cha pesa
kitakuwa kimefikia paundi 100,000/-
Adam anasema anavutiwa sana na Madonna ndiyo maana anafanya kila kitu ili afanane naye.
“Nimewahi
kupanda jukwaani nikamuiga Madonna.. nilipata mashabiki wengi, nimekuwa
nikivutiwa naye kwa kila kitu, nimefanya maamuzi yangu binafsi kwa
kutumia hela zangu ili nifanane naye kutokana na mapenzi yangu kwake,
pia nimepanga kufanya ziara za kimataifa ili kuwadhihirishia watu jinsi
gani navutiwa naye“-Guerra
Social Plugin