Aliyekuwa kiungo wa timu ya Simba SC Christopher Alex Masawe amefariki dunia leo saa 3 Asubuhi katika hospitali ya Milembe mkoani Dodoma baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mama yake mzazi aliyekuwa akimuuguza, maziko yatafanyika keshokutwa siku ya Jumanne.
Christopher
Alex atakumbukwa kwa kufunga penati ya mwisho katika mchezo wa Simba
dhidi ya Zamalek na kuifanya Simba ifuzu hatua ya Robo Fainali ya
michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika mwaka 2003 mchezo uliopigwa
nchini Misri.
Baadhi ya wachezaji waliounda kikosi hicho kilichoitoa Zamalek ni pamoja na Boniface Pawasa, Juma Kaseja na Suleiman Matola.
Rais
wa Simba Evans Aveva ambaye yuko mjini Shinyanga katika pambano la ligi
kuu dhidi ya Stand United ametuma salam za rambirambi kwa familia ya
marehemu na kumuelezea marehemu kuwa aliitumikia Simba kwa juhudi,
mapenzi na uaminifu mkubwa na kusema kwamba Simba itaungana na familia
yake katika msiba huo.
Social Plugin