Mfanyakazi wa
Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na
majambazi wenye silaha na kupigwa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa
fedha zake leo mchana maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar es salaam
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2
alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha
(ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.
Mtandao
huu ulimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuelezea
zaidi tukio hilo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
via>> http://www.williammalecela.com
Social Plugin