Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha
Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya
kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga
kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa
msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na
kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema
ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari
aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa hilo.
Social Plugin