Baadhi ya picha zikionyesha Jengo la ghorofa tatu la Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) lililopo Mtaa wa Moscow na Libya eneo la Posta Jijini Dar
es Salaam linaungua moto.
Moto huo umeteketeza mali kadhaa ambazo bado
haijaulikana thamani yake na kutokana na mashuhuda waliokuwepo wakati
moto huo ukianza kuwaka wanafikiri moto huo huenda umesababishwa na
hitilafu ya umeme lakini msemaji kutoka kikosi cha zima moto amesema
chanzo kamili cha moto huo bado hakijajulikana.
Wasamaria wakiliondoa gari lililokuwa karibu na jengo hilo.
Kikosi cha zimamoto na Jeshi la Polisi wakiwa eneo la tukio.
Social Plugin