Moto
mkubwa uliozuka eneo la Kibangu, Ubungo jijini Dar es Salaam
umeteketeza viwanda vya kusaga plastiki, kuchomelea, useremala na
kuunguza maduka mawili ya karibu pamoja na vibanda vingine vya biashara
eneo hilo.
Watu
walioshuhudia moto huo wamesema moto ulianzia katika kiwanda cha
plastiki na baadaye kusambaa maeneo mengine huku wakilaumu kikosi cha
zimamoto kuchelewa kufika eneo hilo ambapo baada ya kufika walitaka
kuwashambulia kwa mawe lakini Kikosi cha Askari Polisi wakafanikiwa
kudhibiti.
Eneo hilo linazungukwa na makazi ya watu pamoja na kanisa ambayo hayajaathirika na moto huo.
Social Plugin