Ikiwa ni siku moja baada ya
mwili wa mlemavu wa Ngozi Yohana Bahati
mwaka mmoja na nusu kupatikana ukiwa umekatwa baadhi ya viungo,ikiwemo mikono na miguu yote mwili huo
unatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Ibondo kata Katoro Wilayani Geita
Mkoani Geita.
Habari kuhusu Kupatikana kwa mwili wa mtoto huyo
Vilio na Majonzi juzi vilitawala kwa wakazi wa kitongoji cha
Mapinduzi katika Kijiji cha Lumasa jirani na Hifadhi ya Biharamlo Kagera baada
ya kupatikana mwili wa Mtoto Yohana Bahati(mwaka mmoja na miezi sita)ukiwa
umekatwa miguu na mikono.
Mwili wa mtoto Bahati ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino)
huku akiwa amekufa uliokotwa Feb 17 saa 12 jioni na wakazi wa eneo hilo waliokuwa
doria tangu mtoto huyo alipoporwa mikononi mwa mama yake,Feb 15 mwaka huu
kwenye hifadhi yam situ wa Biharamlo Kagera.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo aliieleza Malunde1 blog kuwa mwili huo uliokotwa kwenye shamba la mahindi lililopo katika hifadhi
ya Biharamlo Kagera.
Kwa mjibu wa Kamanda Konyo,mwili huo uliokotwa kwa jitihada
za wakazi wa Kitongoji cha Mapinduzi Kijiji cha Lumasa Wilayani Chato Mkoani
Geita waliokuwa doria wakishirikiana na makachero wa Jeshi la polisi
waliomwagwa huko kwa ajili ya msako wa watu waliohusika na unyama huo.
Kamanda Konyo aliongeza kuwa baada ya mwili huo kuokotwa
ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika hospitali ya
wilaya ya Chato kusubiri uchunguzi na taratibu za mazishi.
‘’Ufuatiliaji wa tukio hilo la mtoto Bahati ambaye ni
mlemavu wa ngozi aliyeibwa Feb 15 saa 2 usiku umefanyika kwa nguvu ya wananchi
na polisi na jana saa 12 jioni tumempata akiwa ameuawa huku amekatwa viungo
vyake miguu na mikono yake yote’’
‘’Mwili huo tumeukuta umetelekezwa kwenye shamba la mahindi
lililopo kwenye hifadhi ya yam situ wa Biharamlo Kagera na tumeuchukua na
kuuhifadhi kwenye hospitali ya Wilaya ya Chato ukisubili uchunguzi na taratibu
za maziko’’alisema Kamanda Konyo.
Kamanda Konyo aliongeza kuwa,tayari jeshi lake linamshikilia
mtu mmoja akihusishwa na tukio hilo ambaye hata hivyo hakumtaja jina lake
kuhofia kuvuruga upelelezi japo alidai kuwepo kwa uhakika wa mtu huyo kujua
ukweli wa tukio hilo.
‘’Tumemkamata mtu mmoja na tunaendelea kumhoji na
tunauhakika kabisa kwamba alihusika na tukio hilo na ni mapema sana kumtaja kwa
ajili ya kutovuruga upelelezi wetu tunaye na tunaendelea kumhoji’’alisema
Konyo.
‘’Lakini kwa kuwa lengo letu lilikuwa kumpata mtoto huyo
akiwa hai kwa bahati mbaya sana tumempata akiwa amekufa na tunawaomba
watanzania wajitafakari na kuchunguza matendo yetu kama yanampendeza mwenyezi
mungu.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Geita Isaack
Timoth mbali na kusikitishwa na kitendo hicho alithibitisha kupatikana kwa
mtoto huyo akiwa amekatwa miguu na mikono.Timoth alisikitishwa na Serikali
kutofanya jitihada za kukomesha matukio ya ukatili wanayotendewa walemavu wa
ngozi kutokana na matukio hayo kuja kwa kasi.
‘’Kinachotupa shida ni kutokana na sheria mbovu zilizopo mtu
mweusi akikamatwa kwa mauaji anahukumiwa lakini Albino anapouawa viungo vyake
vinapelekwa hadi kwa mkemia mkuu jambo ambalo linanifanya niamini serikali
itakuwa inahusika kutokana na kuwalinda watuhumiwa wa mauaji ya walemavu wa
ngozi maana kuna waliokwisha kamatwa na kuachiwa mbali na wananchi kuwatambua
na wengine wamehukumiwa kunyongwa lakini adhabu hiyo haijatekelezwa’’alisema
Timoth
Takwimu zinaonyesha kuwa,katika Wilaya ya Geita kuanzia
mwaka 2007-2012 ni walemavu watano walikwishauawa mpaka sasa na tangu
kuanzishwa kwa mkoa wa Geita ni mlemavu mmoja ambaye ni mtoto Bahati na idadi
yao kufikia sita.
Walemavu hao ni Remmy Juma(2), na Zakaria Juma(7)ambao ni
ndugu wakazi wa Buhalahala kata ya kalangalala mjini Geita.
Wengine ni Rwegamoyo Kitangili wa Kijiji cha Chigunga,Zawadi
Magindu (32)mkazi wa Nyamalulu,Gaspa Elikana wa Nyawilimilwa.
Waliojeruhiwa na kuachwa na vilema 2007-2011 ni Bibiana
Mbushi(9)mkazi wa Nyamwilolelwa alikatwa mguu wa kulia na vidole viwili vya
mkono wa kulia,Nelick Elias(4) wa Kijiji cha Kaseme aliyenyolewa nywele zake na
watu wasiojulikana,Adam Robert(12)mkazi wa Nyaruguguna aliyejeruhiwa mkono wake
wa kushoto na kukatwa vidiole vya mkono wa kulia na kutokomea navyo
kusikojulikana.
Mkurugenzi wa Shirika lisiulokuwa la kiserikali
linalojishughulisha na kuhudumia watoto yatima,Albino na kutoa msaada wa
kisheria la (NELCO),Paulina Alex alidai amepokea kwa masikitiko taarifa za
mwili wa mtoto Bahati kupatikana ukiwa umenyofolewa viungo vyake.
Alex,alisema shirika lake ambalo liliwasaidiwa watoto Albino
80 kupata kiliniki ya magonjwa ymbalimbali huku kati yao 60 wakiwa watoto alilaani
Vikali unyama uliofanywa na watu hao na kuitaka jamii kuachana na imani potofu
kwamba kiungo cha binadamu kinaweza kuwa tiba ya kuelekea kwenye utajiri.
Kwa upande wake
mchungaji Metsoni Asheri wa Kanisa la EAG(T)Tambukaleli mjini Geita aliitaka aliitaka
jamii kuachana na imani potofu za kishirikina kwa kutafuta mali na madaraka kwa
njia ya kuuawa watu na kwamba laana hiyo ni mbaya isipowadhuru wahusika itadhuru
watoto wao.
‘’Ninaomba watu wafanye kazi kwa kutumia maarifa na sayansi
na kama hawawezi wamuombe mungu atawabariki maana yeye ndiye njia ya kweli na
uzima’’alisema Mchungaji Asheri
Tukio la kuibwa kwa mtoto huyo kabla ya mwili wake
kupatikana hiyo jana(juzi)ukiwa umenyofolewa viungo vyake,miguu na mikono
lilitokea katika kitongoji cha Ilyamchele,kijiji cha Ilelema wilayani Chato
mkoani Geita,ambapo watu wasiojulikana walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto
Bahati na kuondoka naye kusikojilikana
huku wakimjeruhi kwa mapanga mama wa mtoto huyo.
Tukio hilo linalohusishwa na imani
za kishirikina lilitokea feb 15 saa 2 usiku na kwa mjibu wa polisi mkoani hapa,Watu
wanaodaiwa kufanya unyama huo walikuwa wawili ambao walivamia nyumbani kwa
wazazi wa mtoto huyo wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye kusikojulikana
baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Kwa mujibu
kamanda wa polisi mkoani Geita,Joseph Konyo,alisema tukio hilo lilitokea saa 2
usiku wakati mama wa mtoto huyo,Ester Jonasi(30)wakati akiwa katika harakati za
kuandaa chakula cha usiku.
Alisema
watu hao wakiwa na mapanga baada ya kufika katika familia hiyo,wamteka mama
yake na katika kunyang'anyana walilazimika kutumia mapanga kwa kumjeruhi mama
wa mtoto huo.
Familia
hiyo inawatoto watatu wote Albino ambapo wakati mtoto mwingine anatekwa kaka
yake alikuwa kwa jirani anacheza na aliporejea nyumbani alikuta tukio
limetokea.
Aidha amesema
baba wa mtoto huyo,Bahati Msalaba anashikiliwa na kwa uchunguzi zaidi kuhusiana
na tukio hilo kwani wakati linatokea alikuwa nje anaota moto(Kikome).
Hili
ni tukio la pili kutokea katika kipindi kisichozidi miezi miwili ambapo Disemba 27,mwaka jana mtoto Pendo Emanule(4)wa Ndami Misungwi
alitekwa na watu wasiojulika na hadi sasa bado hajapatikana wala watekaji wa
mtoto huyo hawajakamatwa.
Na Valence Robert na Victor Bariety- Malunde1 blog Geita