Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.
Akieleza
mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani
na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa
mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.
Kwa
mujibu wa kamanda, mwanamke huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Jenipher
Peter (45).
Alisema alikuwa akiishi na mume wake, Peter Mrosso (43)
pamoja na watoto wao watatu.
Alisema mwili wake ulifukiwa ndani ya boma
la ng'ombe.
Kamanda
alisema taarifa za mauaji ya mwanamke huyo ilitolewa baada ya jirani
yake kupigiwa simu na mume wa marehemu, akimtaarifu kuwa amemuua mkewe
na maiti ameifukia ndani ya boma la mifugo.
Social Plugin