Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWADUI FC YAIBAMIZA POLISI TABORA,SASA KUSHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO

Mashabiki wa Mwadui Fc wakimpa mkono wa pongezi kocha Julio Kiweru kwa kuipandisha Mwadui FC kushiriki ligi kuu msimu ujao-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Awali kabla ya mchezo kati ya Mwadui fc na Polisi Tabora,mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akielekea meza kuu kuketi ili kushudia mtanange huo katika uwanja wa Matete huko Mwadui baada ya kutoa salamu kwa timu hizo na kuwatakia mchezo mwema-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Viongozi mbalimbali wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili kabla ya mchezo huo,mwenye suti nyeupe ni mwenyekiti wa chama cha Mpira mkoa wa Shinyanga bwana Lugola

Wachezaji wakitoa salamu kwa mashabiki kabla ya mchezo kuanza

Golikipa wa timu ya Polisi Tabora akitoa salamu kwa wachezaji wa Mwadui fc kabla ya mchezo kuashiria mchezo uwe wa amani bila vurugu yoyote

Wenye jezi nyeupe ni wachezaji wa Polisi Tabora

Kocha wa Mwadui FC,Msema hovyo Jamhuri Julio Kiweru akiwa kwenye dawati la ufundi akiangalia vijana wake wakisakata kabumbu

Mashabiki wa Mwadui FC wakishangilia ushindi baada ya mchezo kumalizika

Mashabiki wa Mwadui Fc wakimpa mkono wa pongezi kocha Julio Kiweru kwa kuipandisha Mwadui FC kushiriki ligi kuu msimu ujao-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga inayoshiriki ligi daraja la Kwanza leo imeibuka na ushindi wa kishindo kwa kuibamiza Polisi Tabora bao 2-0 katika mchezo wa kufuzu kushiriki ligi kuu bara msimu ujao mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Matete huko Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mwadui FC ilijipatia mabao yake katika kipindi kwa kwanza kupitia kwa mchezaji wake Bakari Kigodeko dakika ya 30 na bao la pili likiwekwa kimyani na Kelvin Kongwe dakika ya 38.

Hadi dakiki 90 za mchezo zikiisha Mwadui Fc ikifanikiwa kulinda magoli yake mawili na kuwafanya kuibuka kidedea katika mchezo huo uliohudhuriwa na maelfu ya wapenzi wa Soka kutoka mkoa wa Shinyanga na maeneo ya jirani kushuhudia mtanange huo.

Kufuatia ushindi huo kocha msema hovyo mwenye maneno mengi Jamhuri Julio Kiweru kutoka Mwadui Fc amewataka mashabiki wa timu yake kuisapoti timu hiyo huku akiahidi kufanya mambo makubwa katika msimu ujao wa ligi kuu Vodacom.
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog- Mwadui Kishapu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com