Polisi wakiwa Muhimbili jana Mwenyekiti wa JKT, George Mgoba akiwa wodini.
Baadhi ya askari wa JKT wakiwasili Muhimbili.
Askari Wakiimarisha Ulinzi eneo la Hospitali ya Muhimbili
KATIBU
wa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa
wakiandamana kushinikiza Serikali kuwapatia ajira, Rinus Emmanuel
amekamatwa jijini Dar es Salaam.
Hatua
hiyo imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wao George Mgoba, kutekwa
wiki iliyopita na kisha kupigwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
Hata
hivyo Mgoba alihamishwa kutoka Hospitali ya Amana, Ilala na kupelekwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambapo anaendelea kupata
mateso kutokana na kutopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Katibu
huyo alikamatwa jana akiwa na wenzake wawili wakati wakiwaongoza wenzao
kwenda kumwona mwenyekiti wao, aliyelazwa katika Hospitali ya
Muhimbili.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari hizi jana, Msemaji wa vijana hao, Omary Bakari alisema katibu wao
alichukuliwa ghafla na polisi walipokuwa wanaingia eneo la Muhimbili
muda mchache baada ya kushuka kwenye gari.
“Hatujui
nini kinaendelea hadi sasa na kwa nini polisi wanatufanyia vitendo hivi
wakijua sisi si wahalifu, tunasikitika sana kwa haya yanayoendelea
kufanyika juu yetu,” alisema Bakari.
Alisema
pamoja na kukamatawa kwa katibu wao na watu waliodai ni askari polisi
wamefuatilia kwa vyombo vinavyohusika ikiwemo polisi lakini wamekuwa
wakipewa majibu ya kukatisha tama, jambo ambalo linawafanya waingiwe na
hofu kuhusu hatima ya kiongozi wao.
Zaidi
ya vijana 300 walikuwa wakiingia hopitalini hapo , huku baadhi yao
wakiwa nyuma ghafla walishuka askari wakiwa wamevaa kiraia ambao
walimvamia katibu wao na kuingia nae katika gari na kutokomea naye
kusikojulina.
Kwa
upande wake Kaimu Mwenyekiti wa vijana hao, Kiwango Mpalare, alisema
kabla ya kwenda Muhimbili walikuwa na kikao chao katika Ukumbi wa
Msimbazi Centre ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hatima ya
kumuuguza kiongozi wao.
“Baada ya kikao wote tulitoka na kuazimia kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kumjulia hali kiongozi wetu.
“Baada
ya kufika hospitali tukiwa zaidi ya vijana 300 walikuja askari wakiwa
katika gari na kumkamata katibu wetu kwa kosa la kukusanyika kinyume cha
sheria. Tunajiuliza wapi tumekusanyika hali ya kuwa tulikuwa kwenye
ukumbi wa mikutano.
“…
je hata katika ukumbi wa mikutano napo kunahitajika kibali cha polisi,
baada ya taarifa hiyo tulifuatilia polisi na kuambiwa kuwa waende
wanasheria kwa ajili ya dhamana. Lakini ilishindika na wote wapo Kituo
cha Polisi Cetral,” alisema Maparale.
Mwandishi
alipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kiliposi Ilala, Mary Nzuki ili
kupata ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa vijana hao alipokea simu na
alipoulizwa swali aliikata.
Hata alipopigiwa kwa mara nyingine zaidi ya mara tatu simu yake iliita bila kupokelewa.
Kutokana
na tukio hilo alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salam, Kamishna Suleiman Kova, alisema bado hajapata taarifa za
kukamatwa kwa vijana hao ambapo aliomba afanye uchunguzi wa kina na
taarifa atatoa leo.
Wiki
iliyopita kiongozi wa vijana hao, Mgoba alitekwa na kisha kuteswa na
watu ambao hawajajulikana, alihamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili
Ijumaa jioni akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa awali.
Mwandishi wa habari alifika Muhimbili jana ikiambata na vijana hao hadi wodi namba sita
jengo la Mwaisela na kumkuta Mgoba amelazwa huku akiwa chini ya ulinzi
mkali wa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za kiraia