Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMME AKUTWA AMEKUFA KWENYE BWAWA HUKO SHINYANGA VIJIJINI ,ALIAGA KWENDA KUJISADIA


Mwili wa Marehemu Charles Makima ukitolewa kwenye Maji hayo-picha na Farajimfinanga.com

Mkazi wa kitongoji cha Nyashimba kijiji cha Solwa, Wilayani Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga, Charles Makima (50-55) amekutwa amekufa maji katika bwawa la Sululuni lililopo katika kijiji hicho.

Mashuhuda wamesema Marehemu Makima amekutwa akielea juu ya maji katika Bwawa hilo jana majira ya saa kumi na moja jioni na ndipo taarifa ilipotolewa kwa wananchi na uongozi wa kijiji kwa ajili ya kuutoa mwili huo ndani ya maji.


Kwa mujibu wa mke wa Marehemu ambaye jina lake halijapatikana mara moja, amesema mumewe alitoka usiku wa kuamkia jana kwenda nje kujisaidia lakini hakurudi tena, na walifanya jitihada za kumtafuta bila mafanikio hadi alipokutwa katika bwawa hilo.

Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika lakini imedaiwa kuwa Marehemu Makima alishawahi kufanya jaribio la kujiua kwa kujikata kisu shingoni mnamo mwaka 1984. 

Hata hivyo baada ya Mwili huo kuopelewa na wananchi, umepelekwa nyumbani kwa Marehemu kuhifandhiwa hadi hapo jeshi la polisi litakapofika kwa ajili ya uchunguzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com