Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Shaban Ramadhan(55)
mkazi wa Ibinzamata mjini Shinyanga ameuawa kwa kukatwa mapanga akiwa amelala
nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus
Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Februari 18 mwaka huu saa nanu usiku
ambapo mwanamme huyo akiwa amelala ndani ya nyumba yake alivamiwa na watu wasiofahamika kisha kumuua kwa kumkata lwa
panga sehemu za shingoni na kichwani.
Amesema katika tukio hilo mtu mwingine aitwaye Sudi
Maige(60) aliyekuwa amelala chumba kimoja na Shaban Ramadhan alijeruhiwa kwa
kukatwa na panga sehemu za usoni na kichwani.
Ameongeza kuwa majeruhi amelazwa katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga kwa matibabu na hali yake ni mbaya na kwamba chanzo cha tukio hilo
bado kinachunguzwa.
Aidha amesema juhudi za kuwabaini na kuwakamata wahusika wa
tukio hilo zinaendelea huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za siri
zitakazowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa waliohusika katika tukio hilo.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin