Kuna namna mbalimbali ya kusupport
harakati, unaweza ukabeba bango lako mwenyewe, au siku hizi teknolojia,
unaweza ukaingia zako tu Twitter halafu unaweka hashtag, basi unakuwa umetoa support yako ya nguvu.
Hawa jamaa wa Uturuki wameona isiwe
tabu, wameingia zao na wenyewe mtaani wakiwa wamevaa zao sketi za
wanawake ili tu ku show support yao ya nguvu kwa wanawake ambao walikuwa
wakiandamana kulaani mauaji ya mwanamke mmoja Ozgecan Aslan ambaye aliuawa na mwanaume aliyetaka kumbaka.
Wanawake wakaingia mtaani kudai haki zao
kwa kuwa kitendo hicho kilionyesha ukatili na unyanyasaji wa wanawake
kwa hali ya juu, wanaume wanaosupport nao wakaongeza nguvu kwa kuvaa
sketi pia na kuandamana.
Social Plugin