Mchezaji wa Stand Abasirim Chidiebele aliyeipatia bao kipindi cha kwanz-picha na Marco Maduhu-Shinyanga |
Timu ya Stand United ya mjini Shinyanga imeinyuka club ya Simba
bao moja kwa nunge katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchezo
ulipopigwa jioni hii katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Goli la Stand United (Chama la Wana) limefungwa na Abasirim Chidiebele kipindi cha kwanza mapema dakika
ya 10 alifunga bao la kichwa kilichomshinda golikipa namba moja wa timu ya Simba
Ivo Mapunda na kutinga moja kwa moja katika nyavu za goli la timu hiyo.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na maelfu ya wapenzi wa soka
kutoka Shinyanga na nje ya Shinyanga ulijawa na vituko vingi ambapo kabla ya
mchezo huo shabiki mmoja wa timu ya Simba aliyefahamika kwa jina la Rajabu Jota alikamatwa na mashabiki wa Stand
United akimwaga dawa katika mlango wa
kutokea wachezaji wa timu ya Stand United.
Kitendo hicho kilisababisha mashabiki wa Stand kumchapa
makofi na makonde kabla ya jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kumchukua
mtuhumiwa.
Baada ya mchezo kuisha kocha mkuu wa timu ya Stand Mathias
Lure ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo na kuahidi kuwa ataendelea kufanya
mabo makubwa katika timu yake.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Simba Golan Kuponovic amesema
Stand siyo timu ya kubeza ni timu nzuri ndiyo maana wameshinda katika mchezo
huo.
Stand sasa wanajiandaa kuikabili Kagera Sukari ambao
wanatumia uwanja wa CCM Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani wakiwa na pointi
18 nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo ambapo Kagera wao wapo nafasi ya 3
wakiwa na pointi 25.
Na Philipo Chimi- Malunde1 blog Shinyanga
BONYEZA MANENO HAYA KUANGALIA PICHA ZA MATUKIO UWANJANI MCHEZO WA SIMBA NA STAND
BONYEZA MANENO HAYA KUANGALIA PICHA ZA MATUKIO UWANJANI MCHEZO WA SIMBA NA STAND
Social Plugin