Martha Nagbe
alijikuta akitozwa faini na Mahakama kwa kesi ya usumbufu na kupigia
kelele majirani na wapita njia, lakini ukweli ni kwamba alipigwa faini
hiyo kutokana na kufanya mahubiri barabarani kwa sauti ya juu na sio
kwamba alikuwa akipiga kelele.
Mke huyo wa mchungaji ambaye amekutana
na mkasa huo Dakota, Marekani amepigwa faini hiyo baada ya kukutwa mara
kadhaa akihubiri barabarani jirani na makazi ya watu ambao nao waliwahi
kulalamika kwamba wanakerwa na kelele za mama huyo, mwisho wa siku
Polisi wa doria walimkuta na kumpeleka Mahakamani ambako alipigwa faini
ya dola 150 ambazo ni zaidi ya 270,000/- Tshs.
Mume wa mwanamke huyo Mchungaji Juwle Nagbe amesema mke wake amesikitishwa sana na maamuzi ya Mahakama hiyo na anauona kama ni uonevu.
Mbali na kupigwa faini hiyo Martha
amesema hatoacha kusali kwa sababu ana imani na MUNGU na pia anaamini
yuko huru kuendelea kufanya mahubiri kwa njia yoyote ambayo ataona iko
sawa na imani yake.
Social Plugin