Picha
ya mwigizaji mkongwe wa vichekesho “KOMEDI” Lucas Mhuvile ‘Joti’
imewakuna watu wengi na kufanya kuwa ni moja kati ya picha zinazo”
TREND” mtandaoni toka jana.
Japo
kuwa Joti akiwa kama ‘Bi kiboga’ ametokelezea kiofisi zaidi, watu wengi
wamejituka wakiangusha komenti nyingi wakielezea kuvunjika kwa mbavu
zao kwa kicheko huku wengine wakisema mnuno wake ndio balaa na wengine wakisema skuna ndio sheedah ilimradi kila mmoja kafurahi kwa mtindo wake.
Kiukweli kabisa kijana huyu ni moja kati ya wakali wa KOMEDI pengine sio hapa bongo tu bali hata Afrika na Dunia .
“Kwanini lakini!!!!!?????? @jotimdebwedo ..Angalau umefanya siku yangu iwe nzuri kidogo leo... ila sio kwa skuna hizo!!!! … kwa kumuangalia tu anapendezea kufanya kazi wapi!? amefanania na ofisi gani!!???? “- Zamaradi Mtetema aliandika haya mara baada ya kuiona hii.