Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI WATUMIA GESI YA PILIPILI KUWAKAMATA WAPENZI WALIOKUWA WANAVUNJA AMRI YA 6 CHOONI

hopps-court-sex_3203953b
Wapenzi wawili, Lee Hops na Hayley McClory  waliokamatwa wakifanya mapenzi kwenye choo cha pub moja mitaa ya Durman, Uingereza wamepandishwa kizimbani kusomewa mashtaka ya makosa mbalimbali.


Siku ya tukio mhudumu mmoja wa aliwakuta na kutoa taarifa Polisi ambao walitumia gesi ya pilipili ili kuwatoa wawili hao na kuwakamata katika choo cha pub ya Wetherspoons.
25CC500700000578-0-image-a-4_1424274502771
Mlango wa Pub ya Wetherspoons

Wanandoa hao wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kupinga amri ya Polisi, kutoa maneno ya vitisho na matusi na kosa la  kumshambulia Polisi na kuchana koti lake.

Hata hivyo walikana mashtaka hayo huku wakilalamika kwamba sheria ilikiukwa kwa wao kupuliziwa gesi hiyo wakati wa kukamatwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com