Bwana Obasanjo amepinga vikali kuahirishwa kwa uchaguzi nchini Nigeria hadi mwezi machi.
Rais
huyo wa zamani amekuwa mstari wa mbele kumkosoa rais wa sasa Goodluck
Jonathan, ambaye anawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha PDP.
Rais Jonathan anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani bwana Muhammadu Buhari.
Muda mchache kabla ya kutimuliwa chamani, Obasanjo aliwaambia
waandishi wa Habari kuwa alikuwa akitarajia kutimuliwa chamani japo
ujumbe ulimfikia mapema kabla ya ya tangazo.
Alichana kadi yake
ya uanachama hadharani jambo lililowaaudhi wandani wa rais kwani ilikuwa
inaonesha mgawanyiko katika chama huku uchaguzi mkuu ukisogea.
Obasanjo amesema kuwa hatojiunga na chama chochote .
"Nitasalia raia wa kawaida ,mimi ni Mnigeria,
Niko tayari kuchangia maendeleo ya taifa kwa ushirikiano wa mtu yeyote bila ya kujali msimamo wa kisiasa.
Hakuna haja ya watu kupanga njama ya kunibumburusha Chamani Chukuwa kadi yenu ya uanachama ,siihitaji'' alisema bwana Obasanjo.
Rais
wa sasa Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kuipigia debe chama
kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC) na mpinzani wake mkuu
Buhari.
Juma lililopita Obasanjo aliliambia gazeti la London
Financial Times kuwa anaomba kuwa rais Goodluck hatofikia kiwango cha
kusema ''asipopata ushindi hakuna atakayeipata''
Rais Jonathan amemkashifu vikali kwa matamshi hayo akisema kuwa Obasanjo anachochea upinzani dhidi ya uongozi wake.
Jeshi
la Nigeria limemlaani Olusegun Obasanjo na kusema kuwa ameliabisha
jeshi kwa kuashiria kuwa walikuwa na njama ya kuongeza muda wa rais
Jonathan.
Bwana Obasanjo ambaye aliyekuwa jenerali wa jeshi na
rais chini ya utawala wa kijeshi aliwaudhi wengi alipodai kuwa
kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ilikuwa ni njama ya rais wa sasa Goodluck Jonathan kutumia jeshi kujiongezea muda wake ofisini.
Obasanjo alipasua kadi yake ya uanachama wa chama tawala PDP hadharani akisema anakihama chama hicho.
via>>BBC
via>>BBC
Social Plugin