Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUKIO LA AJABU MAKABURINI WAKATI WA MAZISHI-MCHUNGAJI NA WAUMINI WAKIONA CHA MOTO


image130
Mhubiri mmoja huko Brazil, Alex Novais de Brito aliyekuwa akifanya mahubiri kwenye mazishi ya muumini wake amejikuta akishindwa kumaliza ibada hiyo baada ya udongo wa kaburi kudidimia na kufanya Mchungaji huyo na waumini wengine watatu kudumbukia kwenye kaburi.

Hilo lilitokea kwenye makaburi ya Campo da Esperanca wakati kukifanyika ibada ya mazishi.

Watu wawili walipelekwa Hospitali ya jirani ili kutibiwa majeraha madogo waliyoyapata baada ya kuanguka, watu walichanganyikiwa baada ya kutokea tukio hilo, Mhubiri huyo alijikuta kwenye wakati mgumu na kushindwa kumalizia ibada.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com