Tunaomba radhi kwa Picha_ BABA AMUUNGUZA MDOMO MWANAE KISA KUDOKOA MAHARAGE


Vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa Wanawake na watoto vinaendelea kushika kasi licha ya Serikali na mashirika mbalimbali ya haki za Binadamu kupiga vita vitendo hivyo kwa nguvu visijiokeze tena.

 Hali hiyo imejitokeza katika kijiji cha Kasaka, Kata ya Nyaruyoba Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma baada ya Baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Sindotuma Nyamubi, kumchoma moto na kumuunguza vibaya sehemu za mdomoni wake, mtoto wake wa miaka saba akimtuhumu kudokoa maharage yaliyotakiwa kutumika kama mboga kwa ajili ya kulia chakula.

Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwa Felix Cosmas amesema kuwa mtoto huyo alibainika kuwa amefanyiwa kitendo hicho baada ya majirani kutomuoana akicheza na wenzake kwa muda wa siku tatu kama ilivyokuwa imezoeleka, ndipo walipogundua alikuwa amefichwa ndani ya nyumba na kugundua tatizo hilo na kutoa taarifa hatua iliyofanikisha mzazi huyo kukamatwa na kufikishwa Polisi.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kibondo,Bi Sofia Gwamagobe amesema kuwa ni vizuri wazazi na walezi kutambua na kujali hali za watoto na sambamba na jamii pia kuendelea kufichua na kutoa taarifa katika vyombo husika ili kuweza kuokoa maisha watu wanaofanyiwa mambo kama hayo kama wamejeruhika kuwapatia matibabu kabla hawajapata madhara makubwa

Hata hivyo Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Kibondo, amekili kuwepo kwa tukio hilo, na kumtaja aliyejeruhiwa vibaya kuwa ni Shukuru Sindotuma na amesema baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa kituoni hapo, amekubali kuwa alimchoma moto mtoto wake kwa kosa la kula maharage bila ruhusa yake

Aidha Baba huyo aliyefanya kitendo hicho ambacho si cha uungwana kwa Mzazi/Mlezi kikufanya kwa Mtoto wake , amehukumiwa kifungo cha miaka mitano Gerezani baada kukutwa na hatia ya Kumfanyia ukatili mtoto wake kwa Kumuunguza mdomoni na kumsababishia maumivu makali .

Nao baadhi wazazi wakazi wa kibondo wamelaani kitendo hicho kilichofanywa na mzazi mwenzao kuwa ni kitendo cha kikatili na kuwataka wanajamii kuacha kutumia hasira kali kwa watoto wadogo

Mtoto huyo Shukuru Sindotuma alikuwa anaishi na baba yake ,mdogo wake mmoja huku Wazazi wao wakiwa wametengana na baada ya kupata Matibabu katika Hopitali ya wilaya ya Kibondo ,amesafirishwa kwenda wilayani Kasulu mkoani Kigoma kwenda kuishi na Mama yake mzazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post