Katika hali isiyo kuwa ya kawaida familia tatu zenye watu 16 katika kijiji cha Mikese mkoani Morogoro wanalazimika kulala nje kwa siku saba mfululizo baada ya nyumba wanazoishi kuwaka moto mara kwa mara na kuunguza samani za ndani na vyakula.
Inaelezwa kuwa chanzo cha moto huo hakifamahamiki na hivyo kusababisha hofu kwa familia hizo kutaka kuyakimbia makazi yao.
Mwandishi wa habari hizi amefika katika familia hizo na kuona vitu mbalimbali
vilivyoungua moto vikiwemo vyakula nguo madaftari ya wanafunzi huku
wakinamama na watoto pamoja na wazee wakiwa nje.
Wananchi hao wamesema katika
hali isiyokuwa ya kawaidia moto huo huwaka zaidi ya mara tisa kwa siku
na wanajaribu kuuzima lakini chanzo cha moto huo hakieleweki ingawa
nyumba hizo hazina umeme wala nishati ya aina yoyote inayosabaisha moto.
Wananchi hao wamefananisha tukio hilo kama la miujiza na kuomba watu wenye
imani mbambali kufika na kufanya maombi katika nyumba hizo kwani
wanateseka kwa kushindwa kulala ndani.
Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Lukole Ramadhani Shaban amekiri kuwepo kwa matukio ya
moto kuwaka katika nyumba hizo kwa siku saba mfululizo.
Amesema
siyo tukio la kawaida na jitihada wanazozifanya kama serikali ya kijiji
wameanza kuwatafuta wachungaji na mashekhe ili kusaidia kufanya
maombi katika nyumba hizo kwani familia hizo zinaishi katika mazingira
magumu ya kulala nje kwa muda mrefu.
Via>>Itv
Via>>Itv