Watuhumiwa wanne wa makundi ya uhalifu waliokuwa wamejificha katika mapango ya maji moto eneo la Amboni jijini Tanga, wametiwa mbaroni na jeshi la polisi kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na wananchi wa kata ya Mzizima ambao wameitikia wito wa jeshi hilo ili kuhakikisha wanaishi kwa usalama.
Habari zilizothibitishwa na viongozi wa jeshi la polisi ambao sio
wasemaji, baadhi ya watuhumiwa ni wenye asili tofauti wakiwemo wenye
asili ya Kiarabu huku wengine wakiwa na asili ya Kisomali ambao wote kwa
pamoja wamekamatwa na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi
hatua iliyosababisha operesheni ya vyombo vya usalama kupunguza kasi
tofauti na ilivyokuwa siku nne zilizopita na kusababisha eneo la tukio
kuwa kimya kuashiria hali inaelekea kuwa shwari.
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wakielezea jinsi
walivyowadhibiti watuhumiwa ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti wakiwa
wamechoka katika vichaka vilivyopo pembeni mwa mapango ya maji moto
yaliyokuwa yakihifadhi wahalifu yaliyopo kilomita 5 kutoka katika yale
mapango ya Amboni yaliyozoeleka ambayo yanamilikiwa kisheria na serikali
kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii, wamesema kukaa na njaa ndio sababu
kuu iliyowafanya kuwakamata kiurahisi kisha kuwapigia simu askari wa
jeshi la wananchi kwa lengo la kuwakabidhi watuhumiwa.
Hata hivyo jitihada za kumpata kamishna wa operesheni wa jeshi la
polisi nchini afande Paul Chagonja ili kutoa taarifa rasmi kuhusu sakata
hilo bado zinaendelea lakini awali amekiri kuwa jeshi hilo litawapa
motisha watu walioshirikia katika zoezi la kufichua wahalifu hatua
ambayo inasubiriwa na wasamaria wema.
via>>ITV
Social Plugin