Je wajua kwanini wanaume wanawapenda wanawake waliojaliwa na makalio makubwa ?
Katika
majarida mengi umewaona wanaume wakikodolea macho picha za wanawake
wenye makalio makubwa iwe ni kim Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj
na Vera Sidika kutoka Kenya .
Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.
Kulingana
na utafiti wa chuo kikuu Bilkent , chuo kikuu cha Texas, na chuo
kikuu cha American University kilichoko mjini Beirut.
Wanaume
wanakisia kuwa mwanamke mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa
bidii zaidi ya mwanamke ambaye hana makalio makubwa.
Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.
Utafiti huo unasema kuwa upinde wa 45.5 ndio unaovutia wanaume zaidi.
Wanaume
walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa
iliwapendelea wanawake wenye makalio yaliyopinda kwa kiwango cha 45.5
Aidha zaidi ya asilimia 30% walisema wangalimchukua mwanamke mwenye makalio makubwa zaidi ya yule waliye naye sasa.
Kwa
mujibu wa utafiti huo katika miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa
na makalio makubwa alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo
mgongoni.
Isitoshe mwanamke kama huyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.
Aidha
mwanamke mwenye makalio makubwa angeweza kustahili uzito wa mtoto
aliyebebwa tumboni na hata kustahilimi makali ya uzazi kuliko wale
wenye makalio wastani.
CHANZO-BBC
Social Plugin