Wanawake wanne kati ya watano
wamekiri wazi kuwa huwa hawaogi kila siku,na wengine wanadai kuwa
wanaweza kukaa kwa siku tatu bila miili yao kukutana na maji.
Utafiti
uliofanywa nchini Uingereza kukagua ngozi za wanawake 2,021 wenye umri
wa kati ya miaka 18 hadi 50 umegundua kuwa mbili ya tatu ya wanawake
wana tabia ya kutoosha nyuso zao zenye poda kabla ya kulala na moja ya
nane ya wanawake pia huwa hawana utamaduni wa kupiga mswaki kabla ya
kulala.
Linapokuja suala la kuoga asubuhi sasa,ni asilimia ishirini
na moja tu ya wanawake ambao hutenga muda wa kuoga asubuhi kila siku,na
asilimia thelathini na tatu ya wanawake huishi kwa siku tatu bila ya
kukutana na maji mwillini mwao.
Jambo la kushangaza mmoja kati ya
wanawake watatu huthubutu kukaa kwa siku tatu bila ya kuosha nyuso zao
pia, kama utashangaa juu ya miili isiyooshwa kwa siku tatu.
Pamoja
na kwamba wataalamu wa masuala ya fya na usafi wa kawaida wa mwili,
asilimia hamsini na saba ya wanawake wa Uingereza wanakiri kutumia
karatasi laini zenye maji maji kujifuta mwilini kabla ya kulala.
Utafiti
uliofanywa uliwafikia wanawake elfu mbili,inaelezwa kuwa asilimia
tisini na mbili wamesema wazi kuwa wanaelewa umuhimu wa utunzaji
ngozi,lakini mtindo wa maisha huwanyima usingizi na ukosefu wa maji
mwilini na hivyo kujiletea madhara kiafya na hasa ngozi zao.
HUWA UNAOGA MARA NGAPI?
Kila
siku? Baada ya siku moja? Mara mbili kwa wiki,mara moja kwa mwezi? Iwe
nataka ama lah,utafiti ukaeleza kuwa asilimia themanini na tisa ya
wanawake wanajitetea kuwa wangependa sana kusafisha miili yao lakini
uchovu wa asubuhi na jioni ndio sababu ya kutooga.
Mmiliki wa
kampuni ya afya ya Flint + Flint Maxine Flint anasema kwamba anaelewa
kuwa wanaojitetea wanadanganya, na kutooga hasa asubuhi haikubaliki
kijamii, kwa watu wanaotuzunguuka na sio afya.
Anasema
tunazungumzia dakika chache unazitumia kuoga kwa siku nzima,inaeleweka
kuwa maisha ya sasa ni haraka haraka lakini kila mmoja pale alipo sio
kweli kwamba hata muda wa kuoga tunaukosa, hatujatingwa kihiivyo.
Kwa
muujibu wa taratibu za afya Maxine anasema ni vyema kusafisha nyuso
zetu kila subuhi na kuukanda kwa joto ili kuchelewesha uzee usoni.Zaidi
ya hayo ,idadi kubwa ya wanawake wanaelewa umuhimu wa utunzaji ngozi
lakini bado hawazitunzi.
via>>BBC
Social Plugin