Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa
manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa
kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajui sababu yake.
Utafiti
uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge
ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano
mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.
Watu wazima hupendelea
kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi
hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na
ule wa kunenepa kupitia kiasi.
Hatahivyo haijabainika kutoka kwa
utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko
kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni
miongoni mwa sababu za magonjwa yasiyojulikana.
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81.
Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.
Baada
ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa
wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya asilimia 46
kupatwa na ugonjwa huo.
Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18
Social Plugin