Mbunge mmoja wa Canada alitoa sababu ambayo haijawahi kusikika iliomlazimu kutoka bungeni kwa haraka.
Amesema kuwa suruali yake ya ndani ndio iliomlazimu kuondoka mapema kwa kuwa ilikuwa ikim'bana.
Mbunge
huyo wa upinzani Pat Martin alimwambia Spika kwamba vazi hilo lilimbana
sana na kumzuia kuweza kuendelea na kikao cha kupiga kura.
Hatahivyo alifanikiwa kurudi kwa wakati na kupiga kura yake.
Baadaye mtandao wa twitter ulijaa ujumbe wa kisa hicho.
Mbunge
huyo alizua ucheshi miongoni mwa wabunge wenzake liposema kwamba
alinunua suruali hiyo kwa bei ya chini bila kujua kwamba ilikuwa ndogo.
Spika wa bunge hilo alisema kwamba alimuagiza mbunge huyo kuketi chini wakati alipotaka kutoka.
Chanzo-BBC
Chanzo-BBC
Social Plugin