Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WAPIGANA MAKONDE,WENGINE WACHAPWA BAKORA WAKATI WA KUMWAPISHA KIONGOZI WAO

Vurugu kubwa imetokea watu kutupiana makonde bakora na silaha zingine za jadi na kusababisha kuvunjika kwa mkutano wa kuwatambulisha viongozi wa serikali ya kijiji cha Mgombani katika miji wa Mto wa Mbu baada ya wananchi kuwakataa viongozi hao kwa madai kuwa siyo chaguo lao hali iliy lilazimu jeshi la polisi kuingilia kati kunusuru usalama katika eneo hilo.

Tukio ilo limetokea katika mkutano ambao uliitishwa na uongozi wa kijiji na kata na baadaye afisa mtendaji wa kijiji cha Mgombani kuanza kuwatambulisha viongozi hao na wananchi kupinga kuzomea na kusoma mwongozo wa uchaguzi kisha kulamamikia ukiukwaji wa taratibu.

Wakizungumza na  mwandishi wa habari wetu wananchi hao walioonekana kuwa na jazba wamesema katika uchaguzi huo mwenyekiti aliyeshinda alikuwa ni mgombea wa Chadema lakini wasimamizi wa uchaguzi walimchakachua na kumtangaza wa CCM wakati matokeo ya awali yalionesha kuwa wa Chadema ndiye aliyeshinda hivyo kamwe awatakubali kuongozwa na uongozi wasiyo uchagua.

Baadaye wananchi waliondoa katika viti viongozi wa serikali ya kijiji na kuwabeba mwenyekiti anayedaiwa kuchakachuliwa pamoja na wajumbe wake na kuwaketisha katika viti ya mbele ya mkutano ambavyo awali walikuwa wamekaa viongozi waliopita kwa tiketi ya CCM.

Kufuatia hali hiyo  kaimu afisa mtendaji wa kata ya Majengo Evarist Mndeme akalazimika kuaihirisha mkutano chini ya ulinzi mkali wa askari polisi huku viongozi waliotambulishwa wakitoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com