Suti
ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh Steven Wassira imegeuka
gumzo mtandaoni baada ya kukosewa kufungwa vifungo vyake.....
Wassira
alionekana ndani ya vazi hilo wakati wa Sherehe za Utume
zilizoandaliwa na kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) na kujumuisha
nchi zingine 11 za Afrika Mashariki na Kati.
Sherehe
hizo zilizofanyika juzi uwanja wa taifa Dar es salaam zilihudhuriwa na
kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted
Wilson ambapo mgeni rasmi wa sherehe hizo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh Steven Wassira (wa pili toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi
wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson(
wa nne toka kushoto) wakati wa sherehe za utume wa kanisa hilo.
Chanzo-Kibonajoro.com |
Social Plugin