Wachimbaji
wadogo wa madini aina ya Dhahabu, walioko katika eneo la Ishinabulandi
katika manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kutoa msaada wa vifaa
kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini hayo pamoja
na mikopo yenye riba nafuu ili kuboresha uzalishaji na kukuza kipato cha
wananchi na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji madini ya
dhahabu ya shinyanga Best,Bw.Kashi Salula ambapo amesema serikali
imekuwa ikiwaahidi mikopo lakini haifawafikii walengwa hivyo kujikuta
wakiendelea kuchimba kwa kutumia dhana zisizokikuwa na tija katika
uzalishaji wa dhahabu.