Wanajeshi
wa jeshi la kujenga taifa-JKT-waliokosa ajira wametoa tamko la kuwataka
wenzao wote walioko mikoani kufika jijini Dar es Salaam kuanzia
Februari 16 ili wajipange kwenda kuonana na rais Jakaya Kikwete
kuwasilisha malalamiko yao baada ya serikali kutumia makampuni binafsi
za ulinzi katika taasisi zake na kuwahacha wao wakizagaa mitaani bila ya
kuwa na ajira.
Wakizungumza na waandishi wa habari wanajeshi hao zaidi ya elfu moja walioko katika mkoa wa Dar es Salaam wamelalamika uamuzi wa serikali wa kutumia makampuni binafsi kulinda taasisi zake na kuwaacha wakiwa hawana ajira wakati wamefanya mafunzo ya kijeshi kwa gharama kubwa za serikali kwa miaka miwili ikiwemo matumizi ya silaha na kutelekezwa mitaani.
Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa umoja wa wanajeshi wa JKT walioko mitaani, Parali Kiwango amesema gharama za kuwahacha askari uraini katika maisha magumu na mazingira yasiyo rafiki ni kubwa kuliko raia kwa kuwa wanaweza kushawishika na kufanya maamuzi magumu.
Chanzo-http://www.itv.co.tz
Social Plugin