Afisa elimu msingi katika halmashauri ya mji wa Kahama
Aluko Lukolela akiwatuliza wazazi waliondamana kwenda shule ya msingi Majengo mjini Kahama
Baada ya Wananchi
wa Mtaa wa Sokola Kata ya Majengo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kufunga kwa
kufuri ofisi ya Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Majengo wakidai ahamishwe, ofisa elimu
Msingi, halmashauri ya mji wa Kahama Aluko Lukolela amesema hatamhamisha badala
yake atampa semina itakayomwezesha kuishi na jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Aluko alisema,
Mkuu wa shule hiyo Japhet Ngulu, amekuwa na uwezo mkubwa wa kufaulisha
wanafunzi, hivyo kumhamisha katika shule hiyo itakuwa ni pigo kubwa licha ya
kwamba anamapungufu ya kutoshirikiana na
uongozi wa kata hiyo.
“Kilichomponza mwalimu ni kiburi chake cha kuwajibu majibu mabaya
viongozi na wazazi wanaofika katika shule hiyo kujua maendeleo ya shule hiyo pamoja na
kushindwa kuwashirikisha kikamilifu katika
miradi ya shule ila taaluma
anaiweza na ndio maana shule hiyo haipishani na shule za Privete” alisema
Lukolela na kuongeza.
“ Mwenyekiti wa mataa huo alikwenda pale zaidi ya mara nne lakini
mwalimu hampi ushirikianao
na wazazi pia wanalalamika
anakauli mbaya kwa wazazi na watoto, kurudisha
manyumbani watoto wasiotoa michango, ambapo hapaswi kumrudisha mwanafunzi
nyumbani ila yeye nanafanya hivyo, kwahiyo unaweza kuona mapungufu
yake yanarekebika.
Alisema tayari ameiagiza kamati ya shule kuitisha mkutano
mkuu utakaoshirikisha wazazi, ndani ya siku 21 ili kujadili mapungufu
yaliyopo katika shule hiyo ambapo kabla ya hapo amepanga kukaa na mkuu wa shule
hiyo ilimpe semina hiyo itakayomwezesha kukaa vizuri na jamii ikiwa ni pamoja
na jinsi ya kushirikisha wazazi katika miradi ya shule.
Wiki iliyopita wazazi walanadamana katika shule hiyo na kuifunga
ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakiishinikiza serikali imhamishe pamoja na kamati
ya shule ivunjwe kwa wameshindwa kushirikiana na wazazi katika miradi ya shule
hali ambayo imesababisha miundombinu ya shule hiyo kuwa mibaya licha ya
michango kutolewa na wazazi.
Wazazi walilalamika pia kutukanwa matusi na mkuu wa shule hiyo pamoja na kuruhusu uchimbwaji wa matundu ya vyoo uendelee wakati wa masika huku wazazi wakitaka ujenzi huo ufanyike wakati wa kiangazi ili kupata vyoo vya kudumu.
Social Plugin