Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WAFUNGA OFISI YA MWALIMU MKUU MJINI KAHAMA,AFISA ELIMU AWATULIZA KIAINA

Afisa elimu msingi katika halmashauri ya mji wa Kahama Aluko Lukolela akiwatuliza wazazi waliondamana kwenda shule ya msingi Majengo mjini Kahama



Baada ya  Wananchi wa Mtaa wa Sokola Kata ya Majengo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kufunga kwa kufuri ofisi ya Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Majengo wakidai ahamishwe, ofisa elimu Msingi, halmashauri ya mji wa Kahama Aluko Lukolela amesema hatamhamisha badala yake atampa semina itakayomwezesha kuishi na jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Aluko alisema, Mkuu wa shule hiyo Japhet Ngulu, amekuwa na uwezo mkubwa wa kufaulisha wanafunzi, hivyo kumhamisha katika shule hiyo itakuwa ni pigo kubwa licha ya kwamba anamapungufu ya kutoshirikiana  na uongozi wa kata hiyo.

“Kilichomponza mwalimu ni kiburi chake cha kuwajibu majibu mabaya viongozi na wazazi wanaofika katika shule hiyo kujua  maendeleo ya shule hiyo pamoja na kushindwa kuwashirikisha kikamilifu  katika miradi ya shule  ila taaluma anaiweza na ndio maana shule hiyo haipishani na shule za Privete” alisema Lukolela na kuongeza.

“ Mwenyekiti wa mataa huo alikwenda pale zaidi ya mara nne lakini mwalimu  hampi ushirikianao na  wazazi pia wanalalamika anakauli mbaya kwa wazazi na watoto,  kurudisha manyumbani watoto wasiotoa michango, ambapo hapaswi kumrudisha mwanafunzi nyumbani ila yeye nanafanya hivyo, kwahiyo unaweza kuona mapungufu yake yanarekebika.

Alisema tayari ameiagiza kamati ya shule kuitisha mkutano mkuu utakaoshirikisha wazazi, ndani ya siku 21 ili kujadili mapungufu yaliyopo katika shule hiyo ambapo kabla ya hapo amepanga kukaa na mkuu wa shule hiyo ilimpe semina hiyo itakayomwezesha kukaa vizuri na jamii ikiwa ni pamoja na jinsi ya kushirikisha wazazi katika miradi ya shule.

Wiki iliyopita wazazi walanadamana katika shule hiyo na kuifunga ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakiishinikiza serikali imhamishe pamoja na kamati ya shule ivunjwe kwa wameshindwa kushirikiana na wazazi katika miradi ya shule hali ambayo imesababisha miundombinu ya shule hiyo kuwa mibaya licha ya michango kutolewa na wazazi.


Wazazi walilalamika pia   kutukanwa matusi na mkuu wa shule hiyo pamoja na kuruhusu uchimbwaji wa matundu ya vyoo uendelee wakati wa masika huku wazazi wakitaka  ujenzi huo ufanyike wakati wa kiangazi ili kupata vyoo vya kudumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com