Wanamme wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kwa tuhuma za kununua
machangudoa katika eneo la Buguruni Rozana jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao waolifikishwa Jumanne ya wiki hii katika mahakama hiyo ni
Antidius Severian (25), Yaham Mihamed (24), Ally Hassan (35) na Mohamed
Hamis (27).
Wakisomewa
mashtaka na wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi Bernard Mpepo, alidai kuwa Februari 14, mwaka huu katika eneo
la Buguruni Rozana watuhumiwa hao walikamatwa na askari mwenye namba
E.7882D/CPL wakifanya manunuzi ya madada poa hao huku wakijua ni kosa
kisheria.
Hata
hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo, ambapo Hakimu Mpepo, alisema
dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi ambapo aliwataka kila mmoja kuwa na
wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini dhamana ya Sh 200,000.
Watuhumiwa
hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi
Februari 24, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.
Social Plugin