Zaidi ya watu hamsini wamekamatwa na jeshi la polisi kufuatia vurugu kubwa iliyotokea katika mji wa Katoro mkoani Geita.
Chanzo cha vurugu hizo ni mgomo wa wanafunzi wa shule za msingi Kilimani, Mkapa na Ludete ambapo walilala katikati ya barabara,
kushinikiza kuwekewa matuta kutokana na matukio ya ajali ya mara kwa
mara hivyo kutishia usalama wao.
Hata baada ya kuwekewa matuta kuzuia ajali vurugu hizo zilipamba
moto kutoka kwa wanafunzi na kuingia watu wazima na kuanza kupiga mawe
magari yote yaliyokuwa yakipita barabarani na zaidi ya magari saba
yameharibiwa vibaya na watu kujeruhiwa.
Baada ya muda kuonekana hali imetulia magari yaliruhusiwa kuondoka
hata hivyo hali haikuwa shwari ambapo magari yote yalirudi kituo cha
polisi Katoro kwa usalama zaidi.
Mkuu wa wilaya ya Geita ameagiza walimu wakuu wote wa shule za
msingi zilizohusika na uanzishwaji wa vurugu hizo kushushwa vyeo vyao na
hatua mbalimbali za kisheria zizingatiwe.
Via>>ITV
Social Plugin