Watu
watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo
dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka
na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es
Salaam.
Kikosi
cha zimamoto walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa
ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta
kama ilivyozoeleka.
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji
wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia
mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza
kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda
miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo
walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema
lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol
Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo
ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.
Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa
majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
Chanzo:ITV
Social Plugin