Watu
watatu wamefariki dunia wakiwemo wakulima wawili na mfugaji mmoja na
watu sita wamejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kwa sime na mapanga kufuatia
mapigano yaliozuka kati ya wakulima na wafugaji katika mbonde la
matembele linaunganisha kijiji cha mabwegere na mbigiri wilayani kilosa
mkoani Morogoro.
Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw Elis Tarimo akizungumzia tukio wakati
alipotembelea majeruhi katika hospitali ya mission St Joseph dumila
amesema chanzo cha tukio hilo ni wafugaji wawili waliwahoji wakulima
waliokua katika shughuli za kutayarisha mashamba kuwa kwanini
hawajafuata taratibu za kujisajili na kuomba kibali kutoka serikali ya
kijiji.
Kufuatia hali hiyo wakulima waliwajibu kuwa wameruhusiwa na mkuu wa mkoa
walime ndipo wakatoa taarifa kwa kundi la wafugaji wapatao 60 ambapo
yakaanza mapigano kwa kutumia mikuki marungu na sime na mapanga
amewataja waliofariki dunia kuwa ni Joseph Peter (26) mkulima ,Rajabu
Selemani (55) mkulima na Kaduru Kashu (30) mfugaji na wengine wamelazwa
katika hospitali na mmoja amehamishiwa katika hospital ya mkoa wa
Morogoro.
Kufuatia tukio hilo mkuu wa wilaya yakilosa Bw Elias Tarimo amesema
tukio hilo la mauji halita vumilika na lazima vyombo vya sheria vifanye
kazi na kuhakikisha watuhumiwa wanakamtwa huku akitupia lawama wizara ya
ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kuchelewa kuleta wasuluhishi wa
mgogoro huo kama walivyoahidi ili kuhakiki upya mipaka ya vijiji ili
kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji iliyodumu kwa muda mrefu.
Nao majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mission St Joseph
Dumila wamelalamikia serikali kushindwa kumaliza tatizo la migogoro ya
wakulima na wafugaji ambapo wameelezea mapigano yalivyotokea.
Naye muuguzi
wa zamu katika hospitali ya mission St Joseph Melania Shayo amesema
wakulima wawili waliofariki dunia wakati wakipatiwa matibu na kukiri
kupokea maiti moja ya mfugaji alieuwawa wakati wa mapigano hayo.
Mapigano haya yamekuja siku chache ambapo nyumba 41 zilichomwa moto
zikiwemo za wakulima na wafugaji kufutia mgogoro wa ardhi katika kijiji
cha Mabwegre wilayani kilosa ambapo mkuu wa wilaya aliwakutanisha
wakulima na wafugaji kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo hata hivyo
mkutano huo uligubigwa na mivutano na wafugaji na kuondoka kabla ya
mkutano kumalizika.
via>>ITV