Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amezungumzia changamoto
alizokumbana nazo kupitia mradi wake wa Kigoma All Stars kwa mwaka 2014
kiasi cha kushindwa kutamba tena.
Akizungumza
na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM leo, Zitto amesema lengo la kundi hilo
kwa mwaka 2014 lilikuwa ni kuwapa uwezo kupitia Saccos yao ambayo
ingewapa fedha ambazo zitawasaidia wasanii wake katika kazi za muziki
wao.
“Mambo
yalikuwa ni mengi, actually mwaka 2013 tulifanya kazi kidogo lakini
2014 hatukufanya kazi kabisa na tulikuwa tunaplan vitu vikubwa na kwa
mfano tulifungua Saccos,” amesema.
“Unajua
moja ya challenge kubwa wasanii wanayo ni anafanya kazi nzuri anahitaji
kurekodi, angalia kama Linex video yake ya Wema kwa Ubaya, ile mwenyewe
asingeweza kwa sababu ya gharama ni kubwa.
Kwahiyo nilikuwa nimeamua
kwanza kuwaanzishia Saccos ambapo kulikuwa kuna fedha pale msanii akiwa
na kazi yake, anatafuta tu mtu wa kutengeneza video na Saccos inalipa
moja kwa moja.
Mapato ambayo anayapata kutokana na ile kazi analipa
kidogo kidogo kwenye ile kampuni ingewafanya wasiwe na wasiwasi kwamba
nitafanya kazi yangu, nitaingia studio nitafanya video bila shida na
ukaingiza kwenye soko,” ameongeza.
“Sasa
hivi inabidi msanii afanye kwanza audio, audio iende then anakuja
anafanya video akishakusanya kusanya hela kidogo, angalia kwenye Wema
kwa Ubaya imetoka audio na video kwa pamoja kwa sababu kulikuwa na mtu
ambaye aliweza kusupport.
Siwezi kusupport wasanii wote kwa muda mmoja,
kwa mfano kuna wasanii ambao nyimbo zao ningependa sana nionyEshe
support, Alikiba wimbo wake wa Mwana, lakini nilishindwa kwa sababu
video ya Alikiba haiwezi kulingana na wimbo wa Linex, ni video kubwa ya
thamani kubwa. Kama unatumia milioni tano kwa Linex kwa Alikiba ni zaidi
milioni kumi na tano. Kwahiyo Saccos ndo ingeweza kusolve matatizo kama
hayo, ndio ilikuwa target yetu kwa mwaka 2014.
“Lakini
2014 ilikuwa na changamoto nyingi. Ni mwaka niliomuuguza mama na
kumpoteza. Mwanzo wa mwaka zilikuwa ni vurugu kutoka kwenye chama changu
cha Chadema, baadaye ndo tumeingia kwenye masuala ya Escrow. Kwahiyo
nikawa nimebanwa muda wote. Kwahiyo hope mwaka huu nitaangalia namna ya
kuwasaidia,” amesisitiza.
“Kuna
watu wana idea nzuri wana nyimbo nzuri, Peter Msechu anahangaika na
wimbo wake wa Nyota, ule ni wimbo unahitaji a lot of promotion lakini
anahangaika mwenyewe.
Najisikia vibaya sana kwa sababu huyu ni mtu
ambaye ningeweza kumsupport na angeweza ku-move on yeye mwenyewe na kuna
wengine ambao hawajatoa tena kazi.
Abdul hajatoa tena kazi, Queen
Dareen hajatoa tena kazi, Makomando hata kusikika sasa hivi hawasikiki,
najua lakini wana kazi mpya lakini ni kazi ambazo tungeweza kuzi-support
zingeweza kwenda mbali zaidi lakini ndo matarajio yangu ya kuweza
kufanya mwaka huu kabla ya uchaguzi.”
Bongo5
Social Plugin