Mtu
mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya basi
la Kampuni ya Saratoga linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Dar es
Salaam, iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kaguruka Kijiji
cha Bweru Kata ya Itebula Wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma, wakati basi
hilo likitoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.
Mganga
wa zamu katika Kituo cha Afya cha Nguruka, Dr.Beatrice Mtesigwa,
amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni Adam Kaimbe mwenye umri
wa miaka 28, mkazi wa Mwanga mjini Kigoma, ambaye ni kondakta wa basi
hilo, ambaye amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika kituo cha
afya cha Nguruka kwa ajili ya matibabu.
Marehemu Adam Kaimbe Enzi za Uhai Wake (Mudy Adamoo)
Amesema
kuwa marehemu amefariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi kupitia
sehemu za puani na masikioni kutokana na kuumia sana kichwani.
“Marehemu
aliumia sana sehemu ya kichwani; tumejitahidi sana kuokoa maisha yake
kadiri ya uwezo wa kituo chetu lakini imeshindikana sababu kichwa chake
kilikuwa kimebonyea na alivuja damu nyingi sana,”alisema Dr.Mtesigwa.
Said Goro ni mmoja wa majeruhi Wawili akiwa Hospitalini
Aidha amewataja majeruhi wa ajali hiyo ni Said Goro mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Kigoma, ambaye amevunjika miguu yote miwili na mkono wa kulia na dereva wa basi hilo Ramadhani Mohamed mwenye umri wa miaka 47, ambaye amepata maumivu sehemu ya mgongo wake.
Aidha amewataja majeruhi wa ajali hiyo ni Said Goro mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Kigoma, ambaye amevunjika miguu yote miwili na mkono wa kulia na dereva wa basi hilo Ramadhani Mohamed mwenye umri wa miaka 47, ambaye amepata maumivu sehemu ya mgongo wake.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Chanzo...KigomaLive