Gari la polisi likiwa nje ya duka hilo
Mashuhuda wakiongea na Malunde1 blog,ambapo wamesema mwanamme huyo amekutwa amefariki dunia wakati akiwa amelala katika duka la mwanamke mmoja aliyejulikana kwa
jina Mama Monica anayefanya kazi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Wamesema Elias alikuwa anafanya kazi ya kuendesha baiskeli
mjini Shinyanga na inapofika usiku alikuwa analala katika duka hilo la madawa
na kwamba alikuwa anaumwa kifua na kutapika damu.
Wakazi wa Ndala wakiwa nje ya duka la Mama Monica
Afisa mtendaji wa kata ya Ndala Dickson Venance amesema
marehemu alikuwa anaishi kwa mmiliki wa
duka hilo kama mlinzi wa duka na alikuwa anaumwa kifua,na kwamba kifo chake kimetokana na kuumwa ugonjwa wa kifua kwa
muda mrefu na inavyoonekana alilala kwenye chumba kisichopitisha hewa.
Baiskeli ya marehemu |
Ndani ya duka la dawa alimofia Elias |
Mama Monica akiwa kwenye gari la polisi akiondoka na polisi na mwili wa marehemu
Wananchi wakiondoka eneo la tukio |
picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Social Plugin