AKUTWA AMEFARIKI KWENYE DUKA LA MADAWA MJINI SHINYANGA


Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Elias(30-34) amekutwa amefariki dunia leo asubuhi ndani ya duka la dawa za binadamu katika mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala mjini Shinyanga-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga


Kushoto ni mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede akiwa ndani ya duka hilo la dawa za binadamu
 Gari la polisi likiwa nje ya duka hilo

Mashuhuda wakiongea na Malunde1 blog,ambapo wamesema mwanamme huyo amekutwa amefariki dunia wakati akiwa amelala katika duka la mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina Mama Monica anayefanya kazi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

 
Wamesema Elias alikuwa anafanya kazi ya kuendesha baiskeli mjini Shinyanga na inapofika usiku alikuwa analala katika duka hilo la madawa na kwamba alikuwa anaumwa kifua na kutapika damu.
 Wakazi wa Ndala wakiwa nje ya duka la Mama Monica
Afisa mtendaji wa kata ya Ndala Dickson Venance amesema marehemu alikuwa anaishi  kwa mmiliki wa duka hilo kama mlinzi wa duka na alikuwa anaumwa kifua,na kwamba kifo chake kimetokana na kuumwa ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu na inavyoonekana alilala kwenye chumba kisichopitisha hewa.

Baiskeli ya marehemu

Ndani ya duka la dawa alimofia Elias

 Mama Monica akiwa kwenye gari la polisi akiondoka na polisi na mwili wa marehemu
Wananchi wakiondoka eneo la tukio
picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم