|
Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa Dr Wilbroad Slaa leo amekabidhi vipande 850 vya mabati vyenye thamani ya shilingi milioni 12 ikiwa ni sehemu ya ahadi ya shilingi milioni 10 zilizoahidiwa na mwenyekiti wa Chama hicho taifa Freeman Mbowe alipowatembelea wahanga wa mvua ya mawe na upepo iliyoua watu 46 katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Mabati hayo yamekabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya(mwenye suti nyesi) leo mchana katika kambi ya wahanga wa mvua hiyo waliohifadhiwa kwa muda katika shule ya msingi Mwakata-picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog |
|
Dr Slaa akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya wakati wa kukabidhi mabati hayo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za waathirika wa mvua hiyo iliyonyesha usiku wa kuamkia Machi 4,2015,mvua ambayo iliua watu wengi,kuua mifugo na kuharibu vibaya mazao |
|
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akimshukuru Dr Slaa kwa kufikisha msaada huo kwa wahanga wa mvua ya Tonado-picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com