ANGALIA PICHA!! DR SLAA AKABIDHI MABATI 850 KWA WAHANGA WA MVUA YA AJABU KAHAMA

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa Dr Wilbroad Slaa leo amekabidhi  vipande 850 vya mabati vyenye thamani ya shilingi milioni 12 ikiwa ni sehemu ya ahadi ya shilingi milioni 10 zilizoahidiwa na mwenyekiti wa Chama hicho taifa Freeman Mbowe alipowatembelea wahanga wa mvua ya mawe na upepo iliyoua watu 46 katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Mabati hayo yamekabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya(mwenye suti nyesi) leo mchana katika kambi ya wahanga wa mvua hiyo waliohifadhiwa kwa muda katika shule ya msingi Mwakata-picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Dr Slaa akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya wakati wa kukabidhi mabati hayo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za waathirika wa mvua hiyo iliyonyesha usiku wa kuamkia Machi 4,2015,mvua ambayo iliua watu wengi,kuua mifugo na kuharibu vibaya mazao

Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akimshukuru Dr Slaa kwa kufikisha msaada huo kwa wahanga wa mvua ya Tonado-picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم